Mapema leo, Kamati ya Ujenzi na Miundombinu chini ya Uwenyekiti wake Mhandisi Bahati Mwaseba, imekabidhi michoro ya ujenzi wa Uwanja wa mazoezi pamoja na Hostel kule Kigamboni
Kamati imekabidhi michoro hiyo baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ya ubunifu ambayo ilifanywa na wataalam walioshirikiana na kamati hiyo
Hatua inayofuata ni ya ujenzi ambapo wakati wowote Yanga itatangaza zabuni kwa zoezi hilo kuanza
Hii ni hatua nzuri kwa klabu ya Yanga kwani baada ya ujenzi wa miundombinu hiyo kukamilika, timu itaweza kutumia miundombinu yake na hivyo kuondokana na gharama za kukodi viwanja kwa ajili ya mazoezi
Ujenzi wa uwanja wa mazoezi umepewa kipaumbele kutokana mahitaji ya klabu wakati huu lakini mradi wote utakapokamilika, Yanga itamiliki Complex yenye mahitaji yote kwa timu ya mpira wa Miguu