Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amewapongeza vijana wake kwa kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba jana Jumapili
Mabao ya Tuisila Kisinda na Waziri Junior yalitosha kuihakikishia Yanga alama tatu muhimu ambazo zimeendelea kuwaweka katika nafasi ya pili kwa tofauti ya lama sita dhidi ya watani zao Simba na alama mbili dhidi ya Azam Fc inayoongoza ligi
Kaze ameeleza kuridhishwa na upambanaji wa vijana wake akiahidi kuwa ushindi huo umeongezea ari na wataendelea kuimarika
"kazi nzuri vijana wamefanya, tutaimarika siku zinazo kwenda. Sapoti ya Wananchii inatukosha Moyo na kututuma tu improve haraka sana. Vijana wamefanya kazi nzuri sana, tutaendelea kuimarika"
"Tunaanza maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Biashara United siku ya Jumamosi," alisema
Kaze amepata ushindi kwenye mchezo wake wa pili tangu aanze kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria