Kaze kuendelea kubadili kikosi kulingana na mechi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Oct 2020
Kaze kuendelea kubadili kikosi kulingana na mechi

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema ataendelea kufanya mabadiliko ya kikosi chake kulingana na mpango wa mechi inayokuja mbele yake

Katika michezo miwili ambayo ameiongoza Yanga na kufanikiwa kushinda yote, Kaze alionekana kufanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake

Mchezo dhidi ya Polisi Tanzania alianza na mshambuliaji mmoja, Yacouba Sogne lakini mchezo dhidi ya KMC akawaanzisha Waziri Junior na Michael Sarpong

Kaze amesema katika kipindi cha siku 12, timu yake inacheza mechi nne hivyo ni muhimu kwa wachezaji kupokelezana majukumu

"Tunacheza michezo minne katika siku 12, hivyo hakuna mchezaji ambaye ana uhakika wa kuanza mechi zote. Baadhi ya wachezaji hawakuwa wamecheza kwa muda mrefu hivyo ni vyema kuwatumia kwa tahadhari kuwaepusha na majeraha"

"Lakini pia uwanja wa CCM Kirumba ni tofauti na uwanja wa Uhuru tuliocheza mchezo uliopita, tulianza na washambuliaji wawili baada ya kubaini hatutakuwa na muda mwingi wa kucheza mchezo wetu, wakati mwingine tulihitaji kutumia mipira mirefu," alisema

Kaze amesisitiza kuwa ligi ya Tanzania ni ngumu hivyo wanapaswa kujiandaa sawasawa kwani hakuna timu nyepesi

Ijumaa ya wiki hii kikosi chake kitakuwa Musoma kuikabili Biashara United katika mechi nyingine ngumu

Biashara United inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 16

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’