Kaze apania kuandika historia Mara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Oct 2020
Kaze apania kuandika historia Mara

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze leo atawaongoza vijana wake katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United ambao utapigwa uwanja wa Karume, Musoma

Huu utakuwa mchezo wa tatu kwa Kaze akiwa ameshinda mechi zote mbili za kwanza tangu akabidhiwe majukumu ya kuinoa Yanga mapema mwezi huu

Lakini pia huu utakuwa mchezo wa tatu kwa Yanga kucheza katika uwanja wa Karume dhidi ya Biashara United

Matokeo ya michezo miwili iliyopita hayakuwa mazuri, Yanga ilipoteza mchezo mmoja na kulazimishwa suluhu ya bila kufungana katika mchezo mwingine

Sio tu Kaze na vijana wake wanasaka ushindi wa kwanza dhidi ya Biashara United hapo Karume, lakini pia Yanga haijafunga bao lolote katika uwanja huo

Hivyo leo Wananchi wamepania kuandika historia kwa kuondoka na ushindi mnonon

Akizungumza baada ya mazoezi yaliyofanyika jana jioni katika uwanja huo, Kaze alisema vijana wake wako tayari kuelekea mchezo wa leo

Kaze alithibitisha kuwa Yanga itamkosa kiungo wake Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambaye ni mgonjwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
41m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
59m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’