Kaze ameanza kuielewa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Nov 2020
Kaze ameanza kuielewa Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema baada ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kwa takribani siku 22, ameanza kuuona mwanga wa timu anayoitaka

Mtaalam huyo wa soka raia wa Burundi amesema wana nafasi ya kuendelea kujiimarisha kama timu na hata mchezaji mmoja mmoja

Kaze amesema matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba hayakuwa mabaya kwa upande wao jambo walihitaji zaidi kuondoka na alama zote tatu

Aidha Kaze ameeleza 'kukoshwa' na sapoti ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuiunga mkono timu yao

"Tumepambana mpaka mwisho lakini matokeo sio tuliyoyatarajia. Baada ya kukaa na timu kwa siku 22 naanza kuona tunaimarika lakini tungali na nafasi ya kujiimarisha zaidi kwa mchezaji mmoja mmoja na timu pia"

"Asante sana Wananchi sapoti yenu jana ilikuwa muhimu sana. Tunarejea kazini kujiandaa na mchezo unaofuata Nov 22 dhidi ya Namungo tuhakikishe tunafanya vizuri," alisema Kaze

Yanga haijapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa msimu huu, imeshinda michezo saba na kutoka sare michezo mitatu

Inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 24

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’