Wakati Tanzania ikiweka kambi nchini Uturuki kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 dhidi ya Tunusia, taarifa mbaya kwa Tanzania ni kuwa nahodha wake Mbwana Samatta hatakuwa sehemu ya mchezo huo utakaopigwa Novemba 13 nchini Tunisia
Taarifa kutoka klabu ya Fenerbahce imebainisha kuwa Samatta ni mgonjwa, madaktari wa klabu hiyo wameshauri apewe mapumziko
Hivyo ni wazi anaweza kukosa mchezo wa kwanza lakini anaweza kuwepo katika mchezo wa pili ambao utapigwa jijini Dar es salaam Novemba 17
Stars iliwasili Uturuki juzi ikiweka kambi ya siku tatu kujiandaa na mchezo huo wa raundi ya tatu kundi J
Stars inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu sawa na Libya wakati Tunisia wanaongoza kundi wakiwa na alama sita
Guinea Bissau inashika mkia ikiwa haina pointi