Winga wa zamani wa Yanga Simon Msuva amesajiliwa na klabu ya Wydad Athletic kwa mkataba wa miaka minne na nusu akitokea klabu ya Difaa El Jadid
Wydad ni moja ya klabu kubwa barani Afrika, wamewahi kutwaa taji la ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho
Msimu huu waliondolewa katika hatua ya nusu fainali ligi ya mabingwa
Juhudi, kujiamini na kujituma ndio silaha anayotumia Msuva kupata mafanikio kila anapokwenda
Mwanzoni aliposajiliwa na Yanga akitokea Azam Fc, Msuva hakuwa na nafasi kubwa lakini jitihada zake zikamfanya baadae akawa mchezaji wa kutegemewa wa kikosi cha Yanga na timu ya Taifa
Kusajiliwa na Wydad ni mafanikio kwake, pia inaweza kuwa njia kuelekea kutimiza ndoto yake ya kusakata kabumbu barani Ulaya
Kwani ndani ya Wydad atakuwa na nafasi ya kuonekana zaidi, timu hiyo inashiriki michuano mikubwa barani Afrika kila msimu