Baada ya mapumziko ya takribani wiki moja, majira ya saa moja usiku wa leo kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kujipima nguvu dhidi ya African Lyon
Mchezo huu ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhid ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumapili ijayo, Novemba 22
Pamoja na kuwakosa nyota wake nane ambao wana majukumu na timu za Taifa, kikosi cha Cedric Kaze bado kimesheheni majembe ambayo yatashuka dimbani kuwapa burudani mashabiki baadae leo
Nyota kama Farouk Shikhalo, Tomombe Mukoko, Zawadi Mauya, Tuisila Kisinda, Sarpong, Sogne, Carlinhos na wengineo kibao watakuwa uwanjani kukonga nyoyo za mashabiki wao
Ni kwa kiingilio cha 3,000/- mzunguko na 5,000/- VIP. Wananchi wameaswa wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono timu yao