Sote tuiunge mkono Taifa Stars - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2020
Sote tuiunge mkono Taifa Stars - Injinia Hersi

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amewahamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 dhidi ya Tunisia

Hersi ambaye ni Katibu wa Kamati ya saidia Stars ishinde, amesema timu ya Taifa ni mali ya Watanzania wote hivyo kuelekea mchezo huo hatupaswi kuwa na matabaka

"Tuache kuweka matabaka yasiyokuwa na tija, tuzipende timu zetu lakini tutambue kuwa zote hizo Mzazi wake ni Tanzania"

"Inapokuwa inacheza Stars inamaanisha ni suala la nchi sio timu hizi mbili pekee, kwahiyo mashabiki wa Yanga na Simba wajitokeze uwanjani na washangilie bila kuwepo matabaka," amesema Hersi

Kesho Jumanne, Stars itakuwa na shughuli pevu mbele ya Tunisia katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za michuano ya Afcon 2021

Baada ya kupoteza mechi mbili zilizopita, Stars inapaswa kupata ushindi ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa michuano hiyo

Guinea ya Ikweta, Libya na Tanzania zote zina alama tatu hivyo kila moja ina nafasi ya kufuzu kama itafanya vizuri katika mechi zilizobaki

Tanzania itacheza mechi mbili nyumbani dhidi ya Libya na Tunisia na baadae kuifuata Guinea ya Ikweta

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
28m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’