Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' usiku wa leo itakuwa na mchezo muhimu wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Afcon 2021 watakapochuana na Tunisia katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa nne usiku
Stars inahitaji kushinda mchezo huu ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa michuano ya Afcon 2021 wakitokea kundi J
Stars, Guinea ya Ikweta na Libya zote zina alama tatu, zikiwania nafasi moja ya kufuzu kuungana na Tunisia ambayo imejikusanyia alama tisa ikiwa inahitaji alama moja tu iweze kufuzu
Kocha Mkuu wa Stars Etienne Ndayiragije amesema kikosi chake kiko tayari kuwakabili Tunisia katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali
Stars itamkosa kiungo Salum Abubakar ambaye alipata majeraha katika mchezo uliopita
Aidha, nahodha Mbwana Samatta nae ataendelea kukosekana akiuguza majeraha aliyopata huko Uturuki
Mashabiki wa soka nchini wameaswa kuweka kando tofauti zao na kuiunga mkono Stars ili kuhakikisha inashinda leo
Mashabiki 20,000 wataruhusiwa kushuhudia mchezo huo ambao hata hivyo unapigwa katika muda ambao sio rafiki sana kwa mazingira ya Tanzania
Kila la kheri Stars..