Kesi ya Morrison iko CAS

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2020
Kesi ya Morrison iko CAS

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick amethibitisha kuwa Yanga ilifanikiwa kufungua kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) wakipinga TFF kupitia Kamati ya Sheria kumtangaza Bernard Morrison kuwa mchezaji huru licha ya kuwa na Mkataba halali na klabu ya Yanga

Akitolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali kutokana na tuhuma zilizopelekwa dhidi yake kuwa ameihujumu Yanga katika sakata la usajili wa Bernard Morrison, Simon amesema baada ya kutokubaliana na hukumu ya kamati ya Elias Mwanjala, walifungua kesi CAS

"Kesi yetu CAS imesajiliwa kwa namba CAS2020/A/7397, hii maana yake ni kesi ya 7397. Ikumbukwe CAS inapokea kesi kutoka kwa nchi Wanachama wa FIFA dunia nzima na ina kesi nyingi sana kama ilivyo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, hivyo msiwe na haraka sana kwenye masuala ya kisheria," alifunguka Simon

Aidha Simon ametolea ufafanuzi wa mashauri manne ambayo Yanga iliyafungua TFF lakini ni kama Shirikisho hilo 'limeyapotezea'

"Sio kweli kwamba mimi nilifuta kesi ya Morrison TFF. Mpaka sasa Yanga ina kesi nne ambazo TFF imeamua kuzipotezea.  Kesi ya Kabwili, kesi ya Morrison kuhongwa dola 5,000 kumshawishi ahame Yanga, kesi ya pingamizi la usajili wa Morrison na kesi ya Mkataba wa Morrison na Simba ambao haujasainiwa na pande zote mbili. Nina ushahidi wa kutosha kuwa kesi hizi hazijasikilizwa na Shirikisho letu la Mpira wa Miguu (TFF)"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’