Fei Toto asawazisha Stars ikilazimisha sare ya Tunisia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2020
Fei Toto asawazisha Stars ikilazimisha sare ya Tunisia

Feisal Salum 'Fei Toto' ameisaidia Tanzania kupata alama moja muhimu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za michuano ya Afcon 2021

Fei Toto alifunga bao hilo kwenye dakika ya 48 akiachia fataki nje ya 18 baada ya kutengewa pasi na John Bocco

Kiungo huyo fundi aliingia kwenye dakika ya 34 kuchukua nafasi ya Himid Mao ambaye hakuwa na mchezo mzuri leo

Hata hivyo ni Tunisia waliokuwa bora kwa muda wote wa mchezo wakipeleka mashambulizi langoni kwa Stars

Walitangulia kufunga bao kwenye dakika ya 11 kupitia kwa Seif Eddine Khoul

Ni matokeo yanayowanufaisha zaidi Tunisia ambao kimahesabu wanaweza kuwa wamejikatia tiketi mapema kushiriki michuano hiyo itakayofanyika Cameroon mwakani

Stars imesogea hadi nafasi ya pili baada ya kufikisha alama nne hata hivyo matokeo ya mchezo kati ya Guinea ya Ikweta dhidi ya Libya yanaweza kubadili msimamo hapo kesho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’