Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema ni faraja kwake kuona hatimaye timu imesimama kileleni mwa msimamo wa ligi na kutaka mashabiki waendelee kuwaunga mkono ili kuhakikisha wanafanikisha malengo ya msimu huu
Kaze amesema katika siku sita zilizopita walikuwa na ratiba ngumu wakicheza michezo mitatu na kufanikiwa kuvuna alama saba kati ya tisa
Amesema mashabiki wanapaswa kuelewa kuwa wachezaji wamepambana katika mazingira hayo magumu kuhakikisha wanawapa furaha ambayo kila mmoja alikuwa akiisubiri
"Bado tunaendelea kuimarisha timu. Wachezaji wanapambana sana kuhakikisha timu inabakia juu"
"Michezo mitatu ndani ya siku sita hakuna mwili wa mchezaji unaweza kuhimili mchakamchaka huo," ameandika Kaze kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii
"Tunacheza na uchovu, maumivu, presha lakini tunafanikiwa kuleta alama tatu kuwapa furaha wananchi"
"Mwananchi popote ulipo unapaswa kuwa na furaha kwani upo juu kileleni, kila mtu anapataka pale na tuko tunapambana sana ili tuendeleee tunafanya vizuri"
"Kwa anayelalamika leo akumbuke tulikotoka miaka mitatu iliyopita. Tunaomba Wananchi mje kwa wingi kutuunga mkoano uwanjani pamoja tutafanikiwa"
"Mchezo unaofuata ni dhidi ya Ruvu Shooting Dec 6th"
Yanga imejichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 31, alama sita zaidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili
Ni alama nane zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya tatu lakini ikiwa na mechi mbili za viporo