Kaze afunguka Yanga kukaa kileleni VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Nov 2020
Kaze afunguka Yanga kukaa kileleni VPL

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema ni faraja kwake kuona hatimaye timu imesimama kileleni mwa msimamo wa ligi na kutaka mashabiki waendelee kuwaunga mkono ili kuhakikisha wanafanikisha malengo ya msimu huu

Kaze amesema katika siku sita zilizopita walikuwa na ratiba ngumu wakicheza michezo mitatu na kufanikiwa kuvuna alama saba kati ya tisa

Amesema mashabiki wanapaswa kuelewa kuwa wachezaji wamepambana katika mazingira hayo magumu kuhakikisha wanawapa furaha ambayo kila mmoja alikuwa akiisubiri

"Bado tunaendelea kuimarisha timu. Wachezaji wanapambana sana kuhakikisha timu inabakia juu"

"Michezo mitatu ndani ya siku sita hakuna mwili wa mchezaji unaweza kuhimili  mchakamchaka huo," ameandika Kaze kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii

"Tunacheza na uchovu, maumivu, presha lakini tunafanikiwa kuleta alama tatu kuwapa furaha wananchi"

"Mwananchi popote ulipo unapaswa kuwa na furaha kwani upo juu kileleni,  kila mtu anapataka pale na tuko tunapambana sana ili tuendeleee tunafanya vizuri"

"Kwa anayelalamika leo akumbuke tulikotoka miaka mitatu iliyopita. Tunaomba Wananchi mje kwa wingi kutuunga mkoano uwanjani pamoja tutafanikiwa"

"Mchezo unaofuata ni dhidi ya Ruvu Shooting Dec 6th"

Yanga imejichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 31, alama sita zaidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili

Ni alama nane zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya tatu lakini ikiwa na mechi mbili za viporo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’