Kaseke ataendelea kuwasha moto VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2020
Kaseke ataendelea kuwasha moto VPL

Kiungo kiraka wa Yanga Deus Kaseke amesema juhudi, kujituma na kufuata maelekezo ya Mwalimu Cedric Kaze ndio sababu ya kuaminiwa katika kikosi cha kwanza

Kaseke aliibuka kuwa nyota wa mchezo katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Azam Fc na JKT Tanzania akifanikiwa kuichangia Yanga alama sita baada ya kufunga bao la ushindi katika kila mchezo

Ni huyuhuyu Kaseke ambaye awali hakuonekana kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga. Lakini tangu alipowasili Kaze mambo yameanza kumnyookea

Aidha, Kaseke ametengeneza maelewano mazuri na mshambuliaji Yacouba Sogne ambaye ndiye aliyetengeneza mabao yake yote

Nyota huyo wa zamani wa klabu za Mbeya City na Singida United, ameeleza kutambua aina ya uchezaji wa Sogne na anaamini ataendelea kufunga kama wataendelea kutumika pamoja

"Mimi na Yacouba tumekuwa tukielewana hata tunapokuwa mazoezini, nishafahamu anacheza kwa mtindo gani, hata na yeye pia anafahamu mimi nachezaje

"Ndio maana mara nyingi mipira anayoshika inatoka kwangu, na mimi nikipata mpira kwenye eneo la hatari, mara nyingi huwa inatoka kwake.

"Naamini kama mwalimu ataendelea kutuamini, nitakuwa nafunga au kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambayo yatatupa pointi ambazo sisi tunazihitaji kwa ajili ya kuwania ubingwa msimu huu," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’