Yanga na Simba ni watani, sio mahasimu

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
3 Dec 2020
Yanga na Simba ni watani, sio mahasimu

Kauli ya msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara kuwakataza mashabiki wa soka wasiokuwa wa klabu yake kuhudhuria mchezo wa ligi ya mabingwa mwishoni mwa wiki watakayocheza dhidi ya Plateau United, haipendezi na inaweza kusababisha madhara

Kwa miaka mingi vilabu vya Yanga na Simba vimekuwa na utamaduni ambao kwa kiasi kikubwa ndio unaonogesha upinzani uliopo

Kwa Tanzania haitatokea mashabiki wa Yanga wakaiunga mkono klabu ya Simba katika mashindano yoyote, iko hivyo hata kwa upande wa Simba

Suala la mashabiki wa timu moja kuingia uwanjani kuwashangilia timu pinzani kwa mechi zinazozihusu Yanga na Simba, ni kawaida kabisa

Sio jambo lililoanza leo, imekuwa hivyo kwa miaka mingi na huko nyuma hakukuwahi kutokea tatizo lolote

Sasa inapofika wakati kiongozi wa timu moja anajitokeza hadharani anatangaza kuwa kwenye mchezo wetu hatuwataki mashabiki wa timu nyingine ni jambo ambalo linaweza kuwa gumu kutekelezeka

Hivi itakuwaje kama Yanga na timu nyingine nazo zikitangaza kuwa hawawataki mashabiki wa Simba kwenye mechi zao? hatuoni kama tunapoelekea tunaenda kutengeneza uhasama?

Ni bahati mbaya sana kipindi hiki baadhi ya viongozi wa mpira kwa makusudi kabisa wanaamua kutupeleka mashabiki sehemu ambayo hatupaswi kwenda

Naamini tamko la Manara alilitoa yeye kama yeye na hakutumwa na Taasisi anayoifanyia kazi

Kwani itakuwa aibu kwa Taasisi kubwa kama Simba inayojitamba kuendeshwa kisasa zaidi kuliko wengine nchini kufanya kile kilichozungumzwa na Manara

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’