Ntibazonkiza aahidi kunogesha vita ya ubingwa Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Dec 2020
Ntibazonkiza aahidi kunogesha vita ya ubingwa Ligi Kuu

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza ameeleza kufarijika na mapokezi aliyopewa na Wananchi juzi baada ya kutua akitokea kwao Burundi

Aidha nyota huyo aliyejijengea heshima ya kipee katika soka la Burundi, amesema atahakikisha mchango wake unaisaidia Yanga kutimiza malengo ya kushinda ubingwa

Amebainisha kuwa wakati yuko kwao akisubiri kujiunga na Yanga, alikuwa akifuatilia ligi kuu na anaamini Yanga imestahili kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwani wana kikosi imara zaidi kulinganisha na timu nyingine

"Asante mashabiki wa Yanga kwa mapokezi makubwa. Najua nina deni kubwa hapa, naahidi nitawapa furaha tukishirikiana na wachezaji wenzangu wa Yanga," alisema

"Nimekuwa naangalia kweli mechi za timu mbalimbali wakati nikiwa nyumbani, naona Yanga ni timu bora ambayo inastahili kuwa juu ya msimamo, hatua hii ya kuongoza ligi ni kitu kikubwa nafasi yangu sasa ni kutumia uzoefu wangu kuongeza kitu nikishirikiana na wenzangu katika kuipa mafanikio timu yangu mpya," alisema

Ntibazonkiza alianza kujifua na kikosi cha Yanga jana Alhamisi, akitarajiwa kuanza kuonekana akiwatumikia mabingwa hao wa kihistoria baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili Disemba 15

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’