Kwa huyu Fei Toto wasahau..

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Dec 2020
Kwa huyu Fei Toto wasahau..

Afisa Habari wa zamani wa klabu ya Yanga ambaye kwa sasa ni Afisa Masoko, Dismas Ten 'amewapiga dongo' Simba kuwa harakati zao za kujaribu kumsajili kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' haziwezi kufanikiwa

Kwa nyakati tofauti imeelezwa kuwa Simba inamnyemelea Fei Toto kwa mbinu zilezile walizotumia kumnasa Bernard Morrison

Mwanzoni mwa msimu Yanga kupitia wadhamini GSM, walimpa Fei Toto mkataba wa miaka minne akiwa pengine ndiye mchezaji mwenye mkataba mrefu zaidi nchini

Ten amefichua kuwa Simba wamejaribu kuwasiliana na wazazi wa nyota huyo katika jitihada za kutaka kumshawishi ahamie upande wao. Amewapiga dongo kuwa wasijisumbue kwani hawana hela ya kumsajili Fei Toto

"Simba haina hela ya kumsajili Fei Toto, mnahangaikatu mara kwa mama ake mara kwa mjomba ake Feisal Salum hauzwi," aliandika Ten kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Kwa miaka ya karibuni Simba imetumia changamoto za kiuchumi zilizoikabili Yanga kusajili wachezaji kutoka Yanga jambo ambalo kwa sasa haitakuwa rahisi kutokea baada ya timu kuwa chini ya GSM. Aidha sakata la Bernard Morrison limewaongezea umakini zaidi viongozi wa Yanga

Juzi mshambuliaji Saido Ntibazonkiza alifichua kuwa viongozi wa Simba walijaribu kumshawishi aachane na mpango wa kujiunga na Yanga ili wamsajili ashiriki michuano ya Kimataifa

Hata hivyo nyota huyo kutoka Burundi aligoma na kuwataarifu GSM na viongozi wa Yanga juu ya watu hao waliokuwa wakimsumbua

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’