Ruvu Shooting watakumbana na 'mziki' kamili wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Dec 2020
Ruvu Shooting watakumbana na 'mziki' kamili wa Yanga

Keshokutwa Jumapili Disemba 06, Yanga itashuka pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Huu ni mchezo mihimu kwa timu ya Wananchi kukusanya alama nyingine tatu ambazo zitazidi kuwakita kileleni mwa msimamo wa ligi

Baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao Yanga ilishinda kwa bao 1-0, vijana wa kocha Cedric Kaze walipata muda wa wiki nzima kujiandaa na mchezo huu

Kabla Yanga ilikabiliwa na ratiba ngumu, ikicheza mechi tatu katika kipindi cha siku sita

Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania, wachezaji wa Yanga walionekana kuchoka hasa kwenye kipindi cha pili, Kaze alitaja sababu kuwa ilitokana na uchovu wa kucheza mechi mfululizo

Sasa Jumapili Ruvu Shooting watakumbana na Yanga ambayo iko 'fresh', utakuwa mchezo ambao walinzi wa Ruvu Shooting watakuwa 'busy' kupambana na kasi ya kina Tuisila Kisinda, yacouba Sogne na Deus Kaseke ambaye yuko kwenye kiwango bora sana

Lakini pia, nahodha Lamine Moro anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kutumikia kadi tatu za njano

Siku hiyo Wananchi pia wanaweza kumshuhudia Haruna Niyonzima 'Baba mzazi' ambaye mchezo uliopita hakupewa nafasi kwa kuwa alichelewa kurudi kutoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa baada ya kupata ajali nchini Rwanda

Kama kawaida yake, Msemaji wa Ruvu Shooting Massau Bwire tayari ameanza tambo zake, akidai kuwa watatoa haki sawa baada ya kuwafunga Simba basi itakuwa zamu ya Yanga

Bwire anapata jeuri ya kutamba kutokana na uimara wa kikosi cha Ruvu Shootinga msimu huu

Maafande hao wanaonolewa na kocha Charles Mkwasa 'Master', wanashika nafasi ya nne wakiwa wamejikusanyia alama 23 sawa na Simba wakizidiwa mabao tu

Ruvu Shooting ni moja ya timu zinazocheza kandanda safi msimu huu, bila shaka mashabiki watashuhudia burudani ya aina yake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’