TK Master, winga mwenye kasi ya upepo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2020
TK Master, winga mwenye kasi ya upepo

Hakuna shaka jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting, nyota wa mchezo alikuwa ni mmoja tu, Tuisila Kisinda 'TK Master'

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mabao yote ya Yanga yalipita mguuni kwa TK Master

Baada ya Bernard Morrison kuondoka Yanga na kujiunga na Simba katika mazingira ya kutatnisha, wapo waliopata hofu kuwa kuondoka kwake pengine kungeiathiri Yanga

Lakini sidhani kama kuna Mwanayanga ana hata huo muda wa kumfikiria Morrison, ujio wa Kisinda umemfuta kabisa Morrison katika mioyo ya Wananchi

Kisinda amerejesha ule utamaduni wa Yanga kushambulia kupitia pembeni, kasi yake imekuwa changamoto kwa walinzi ligi kuu

Mpaka sasa TK Master amedhihirisha kuwa hakabiki, huyu mwamba ana kasi mithiri ya upepo. Amefanikiwa kuitumia silaha hiyo kuwatesa walinzi wa timu pinzani

Mlinzi wa Simba Joash Onyango 'Babu Onyango' ni miongoni mwa walioonja shubiri ya Kisinda! Jana walinzi Cassian Ponera na Juma Nyosso nao hawakukiepuka kikombe hicho

Mpaka sasa Kisinda amehusika kwenye mabao manne ya Yanga, akifunga moja na kutengeneza mabao matatu

Kadiri anavyoizoea ligi ya Tanzania, ndivyo anavyoendelea kuwa hatari zaidi

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
42m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’