Uongozi wa Namungo Fc wamethibitisha kuwa wamezuiwa kumtumia kiungo wa Simba Shiza Kichuya ambaye jana alitangazwa kufungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa miezi sita baada ya kubainika usajili wake kwenda klabu ya Simba haukufuta taratibu
Aidha klabu ya klabu ya Simba imepigwa faini ya dola 130,000 na wametakiwa kulipa fedha hizo katika muda walioelekezwa ili waepuke kifungo
Ofisa Habari wa Namungo Fc Kidamba Namlia amethibitisha kupokea taarifa kutoka FIFA ikiwazuia kumtumia Kichuya ambaye walimsajili kwa mkopo kutoka klabu ya Simba
Namlia amesema Simba wanaweza kufungiwa kusajili kwa miaka mitatu kama hawatalipa faini hiyo kwa wakati waliopewa
"Tumeambiwa na FIFA kwamba tusimtumie mchezaji (Kichuya) mpaka pale Simba itakapolipa faini, ikiwa itashindikana kulipa basi itafungiwa kufanya usajili kwa muda wa miaka mitatu," alisema