Leo ilikuwa siku nzuri sana kwa mshambuliaji Yacouba Sogne ambaye amechangia ushindi wa mabao 5-0 iliyopata Yanga dhidi ya Mwadui Fc
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga, Yacouba alifunga mabao mawili na pia akatoa pasi mbili za mabao yaliyofungwa na Deus Kaseke na Tuisila Kisinda

Katika mchezo wa nne mfululizo, mguu wa Yacouba unasababisha ushindi muhimu kwa Yanga
Hongera kwa kocha Cedric Kaze ambaye sasa anaonekana kupata kanuni inayowafanya washambuliaji wake waanze kuonyesha makali yao
ADVERTISE HERE