Kiungo wa YangaBalama Mapinduzi amekamilisha awamu ya kwanza ya matibabu baada ya kukamilisha vipimo nchini Afrika Kusini
Balama ataingia awamu ya pili ya matibabu yake kuanzia kesho
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema awamu ya kwanza ilikuwa ni vipimo vya aina tatu , ambavyo vimekamilika
Kinachofuata ni Madaktari kuona matibabu gani yanafaa baada ya kujiridhisha na majibu ya vipimo
Bumbuli amesema madaktari wamegundua kwamba mfupa uliunga vibaya hali ambayo ilikuwa ikimsababisha maumivu aliyokuwa akiyapata wakati alipoanza mazoezi mepesi
ADVERTISE HERE