Yanga imepata mtu! ndivyo wadau wanavyosema baada ya kumshuhudia nyota mpya Sadio Ntibazonkiza akitupia kambani mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 ambao Yanga imepata dhidi ya Singida United
Ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza tangu alipojiunga na Yanga wiki mbili zilizopita
Ntibazonkiza amedhihirisha ni mtu haswa, ana jicho kali la kuliona lango lakini pia pasi zake, kina Michael Sarpong, Yacouba washindwe wenyewe tu
Wakazi wa Singida leo wameshuhudia burudani ambao wameikosa kwa miezi kadhaa tangu timu yao ilipoteremka daraja
Aliyekamilisha idadi ya mabao kwa Yanga alikuwa Deus Kaseke ambaye kwa sasa yuko kwenye kiwango bora sana, akiweka kambani bao safi dakika chache baada ya kuingia
Huu mziki wa Yanga, timu zijiandae raundi ya pili kutakuwa na vipigo vingi vya mbwa koko!



