Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Yanga leo wako mkoani Arusha saa kumi jioni wakitarajiwa kushuka katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili Dodoma Jiji
Ni mwendelezo wa mechi za ligi kuu sasa ikiingia raundi ya 16
Kwa Yanga kila mchezo ni kama fainali, mahitaji ya ushindi ni suala la lazima ili kuhakikisha mwishoni mwa msimu wananchi wanashangilia ubingwa wa 28
Wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani wameipokea timu yao kwa shangwe hapo juzi, jana walijitokeza kwa wingi kushuhudia mazoezi ya mwisho
Dodoma Jiji leo watakuwa na kazi ya ziada kuizuia Yanga ambayo iko katika kiwango bora sana
Vijana wa kocha Cedric Kaze wameshinda mechi nne mfululizo mchezo uliopita wakiwafumua Mwadui Fc mabao 5-0
Aidha, leo Wananchi wanaweza kumshuhudia mshambuliaji mpya Saido Ntibazonkiza akicheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi
Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa tayari wamepokea leseni ya Ntibazonkiza hivyo yuko tayari kwa mchezo huo
Mchezo utaunguruma kuanzia saa kumi Alasiri