Yanga Sc na Yanga Princess zimeendelea kukimbiza ligi kuu ya Vodacom na ligi Kuu ya Wanawake 'Setengeti Lite' zikibaki kileleni mwa misimamo ya ligi hizo
Baada ya misimu mitatu ya changamoto za hapa na pale, Wananchi wamepania kwelikweli, mwendo ni huu huu hadi kieleweke!
Wakiwa wameshuka dimbani mara 16, Yanga wanaume wamekusanya alama 40, wakiwa kileleni kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili
Dada zao nao wanakimbiza ligi ya Wanawake wakikusanya alama 16 baada ya kushuka dimbani mara nane


ADVERTISE HERE