Ujumbe uwafikie wale wachambuzi 'uchwara'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Dec 2020
Ujumbe uwafikie wale wachambuzi 'uchwara'

Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewatolea uvivu baadhi ya wachambuzi ambao wanahoji idadi ya mabao ambayo washambuliaji wa Yanga wamefunga bila ya kujali mchango wao katika mafanikio ya kikosi cha Yanga mpaka sasa

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Bumbuli ameandika haya;

Kumekuwa na mjadala juu ya washambuliaji wa Yanga, kwamba hakuna mwenye mabao mengi. Huu ni mjadala ambao umetokana na MSHUTO wa nafsi za baadhi ya wachambuzi wetu ambao awali walitoa maoni yao kuwakashfu na kuwakejeli washambuliaji wetu

Awali nilisema na kusisitiza kwamba Yanga tunaimani kubwa na washambuliaji wetu, na kamwe kama uongozi hatukuruhusu siasa za wachambuzi kuingia vichwani mwetu juu ya ushindi wa bao moja moja tuliokuwa tukiupata.

Taratibu safu ya ushambuliaji ilijengwa na kuimarika, washambuliaji wetu wamefunguka, wanafunga na kutengeneza nafasi kwa wengine

Katika mechi tatu za mwisho safu ya ushambuliaji imetengeneza mabao 11 na kufunga nane, kati ya mabao 11 ambayo Yanga imevuna, mabao matatu yamefungwa na mabeki na moja limefungwa na kiungo Feisal Salum.

Hadi sasa Yanga tumefunga mabao 28 na kuruhusu mabao sita, kwa umoja washambuliaji, viungo na mabeki wamefanikisha kukusanya pointi 43.

Tupo kileleni na timu inaendelea kuimarika chini ya Kocha Cedric Kaze na benchi lake la Ufundi.

Usajili wetu msimu huu hatukuzingatia wingi wa mabao ambao wachezaji walikuwa nao, tuliangalia uwezo wa washambuliaji na kile ambacho watakileta kwenye timu yetu

Tulijua Michael Sarpong anauwezo wa kufunga lakini hakuwa amecheza kwa miezi sita, tulijua wazi Yacouba Songne hakuwa mfungaji bora alikotoka, lakini tuliamini katika uwezo wake.

Hivyo basi tungetaka kusajili mfungaji bora, bila shaka tungepata washambuliaji ambao waliongoza katika ligi zao. Tulijua tunahitaji nini kutoka kwa wachezaji tuliowasajili, ndio maana tunasubira na tunaridhika na kile kinachoendelea kwenye kikosi chetu mpaka sasa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’