Kiungo wa Yanga Carlinhos amepewa program ya mazoezi kujiweka sawa kabla ya kurejea uwanjani mwaka 2021
Tangu atue Yanga, Carlinhos amekosa mwendelezo mzuri wa kucheza kutokana na majeraha yanayomsumbua mara kwa mara
Imeelezwa wakati anajiunga na Yanga nyota huyo hakuwa fit, kwani hakucheza soka la ushindani katika kipindi cha miezi sita huko kwao Angola baada ya ligi ya nchi hiyo kufutwa kutokana na changamoto ya ugonjwa corona
Katika mechi alizocheza, Carlinhos amekuwa mhanga wa kufanyiwa madhambi. Walinzi wa timu pinzani wanamkamia sana na hivyo kumfanya apate majeraha mara kwa mara
Benchi la ufundi la Yanga linaloongozwa na kocha Cedric Kaze wamempa program ya mazoezi anayoendelea nayo jijini Dar es salaam wakati wenzake wakiwa mkoani Mbeya wakijiandaa na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons
Carlinhos amepewa program ya kuimarisha utimamu wa mwili akianza kwa kufanya mazoezi ya Gym
Kiungo huyo fundi anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachokwenda visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza wiki ijayo