Ni heshima kuitwa timu ya Taifa - Yassin

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jan 2021
Ni heshima kuitwa timu ya Taifa - Yassin

Mlinzi wa kushoto wa Yanga Yassin Mustafa ameeleza furaha yake baada ya kuitwa timu ya Taifa kwa mara ya kwanza

Yassin ni miongoni mwa wachezaji sita wa Yanga waliojumuishwa katika kikosi cha Stars kinachokwenda nchini Cameroon kushiriki fainali za CHAN zinazohusisha wachezaji wa ndani

"Ni ndoto ya kila mchezaji kuichezea timu yake ya Taifa kwani naamini huwezi kujiita mchezaji uliyefanikiwa sana kama hukuwahi kuitumikia timu ya Taifa. Hivo kwangu mimi ni jambo la furaha na heshima kubwa kuitwa kulitumikia Taifa langu," alisema Yassin

"Ninachohitaji kutoka kwa mashabiki ni kuungwa mkono. Watuunge mkono wachezaji wote tulioitwa timu ya taifa kwani sote tunakwenda kufanya kazi moja, kuipa heshima nchi yetu," alisema Yassin

Nyota wengine wa Yanga waliojumuishwa katika kikosi hicho ni Bakari Nondo Mwamnyeto, Feisal Salum,Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Farid Mussa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
42m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’