Kaze, Ntibazonkiza washinda tuzo VPL Disemba 2020

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2021
Kaze, Ntibazonkiza washinda tuzo VPL Disemba 2020

Kocha Mkuu wa Young Africans SC ya Dar es Salaam, Cedric Kaze amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Disemba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2020/21, huku Saido Ntibazonkiza wa Young Africans pia akichaguliwa Mchezaji Bora wa mwezi huo.

Saido na Kaze walitwaa tuzo hizo baada ya kuwashinda wenzao walioingia nao fainali kwa mwezi Disemba katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na Kamati ya Tuzo za VPL, kutokana na mapendekezo ya makocha waliopo vituo mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.

Kwa Disemba, Saido aliwashinda kiungo Clatous Chama wa Simba na kiungo mshambuliaji wa Dodoma Jiji FC, Seif Karihe alioingia nao fainali huku Kaze akiwashinda Sven Vandenbroeck wa Simba na Francis Baraza wa Biashara United.

Yanga chini ya Kaze kwa mwezi huo ilishinda michezo minne na kutoka sare mmoja ikivuna pointi 13 na kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi. Yanga ilizifunga Ruvu Shooting FC (2-1), Mwadui FC (0-5), Dodoma Jiji FC (3-1) na Ihefu SC 0-3 huku wakitoka sare na Tanzania Prisons FC 1-1.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
48m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’