Dirisha dogo la usajili litafungwa kesho Ijumaa saa 5:59 usiku, ahadi ilitolewa kwa Wananchi juzi na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Injinia Hersi Said kuwa wajiandae kwenda JNIA kupokea mshambuliaji wa kigeni kabla ya dirisha hilo kufungwa
Baada ya ushindi wa michuano ya kombe la Mapinduzi jana, furaha ya Wananchi leo inaweza kunogeshwa zaidi na usajili wa kibabe unaotarajiwa kufanywa na GSM kuja kumaliza changamoto katika safu ya ushambuliaji
Yanga imepania kushinda mataji yote msimu huu, maboresho ya kikosi hasa safu ya ushambuliaji ni jambo la lazima, GSM wamekisikia kilio cha Wananchi bila shaka ujio wa mshambuliaji huyo utakuwa chachu na kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji
ADVERTISE HERE