Msafara wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' umeondoka Alfajiri ya leo kuelekea nchini Cameroon kushiriki fainali za michuano ya CHAN inayoanza nchini humo keshokutwa Jumamosi, Januari 16
Kabla ya kuianza safari, Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Abdallah Ulega aliikabidhi timu hiyo bendera ya Taifa
Hii ni mara ya pili Tanzania inapata nafasi ya kushiriki fainali za michuano hiyo wakipangwa kundi D pamoja na nchi za Zambia, Namibia na Guinea
Itashuka dimbani kucheza mechi yake ya kwanza Jumanne Januari 19 dhidi ya Zambia, Januari 23 watacheza na Namibia na watakamilisha hatua ya makundi januari 27 kwa mchezo dhidi ya Guinea
ADVERTISE HERE