Shikhalo, Makapu, Ninja wampa mtihani Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jan 2021
Shikhalo, Makapu, Ninja wampa mtihani Kaze

Kiwango kizuri kilichoonyeshwa na walinzi Said Juma Makapu na Abdallah Shaibu 'Ninja' katika michuano ya kombe la Mapinduzi kimempa mtihani kocha Cedric Kaze

Awali kulikuwa na tetesi kuwa mmoja wao angetolewa kwa mkopo baada ya usajili wa mlinzi Dickson Job kutoka klabu ya Mtibwa Sugar

Lakini ni wazi nyota hao walion'gara kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Simba, wamempa wakati mgumu Kaze kuamua nani atamtumia katika kikosi chake cha kwanza

Yanga sasa ina walinzi watano wa kati ambao yeyote anaweza kutumika katika mchezo wowote

Katika duru ya kwanza Kaze aliwatumia zaidi manahodha Bakari Nondo Mwamnyeto na Lamine Moro lakini sasa Makapu na Ninja wamemhakikishia kuwa nao wako imara wakati huohuo akiwa amemsajili beki kisiki Dickson Job

Aidha mlinda lango Farouk Shikhalo ambaye aliibuka kuwa kipa bora wa michuano ya kombe la Mapinduzi nae anaweza 'kupindua meza' mbele ya Metacha Mnata

Shikhalo alikuwa na kiwango kizuri katika michuano hiyo akiruhusu bao moja tu lakini pia akionyesha uhodari mkubwa katika kudaka mikwaju ya penati

Benchi la ufundi watakuwa na mtihani kuamua nani aanze kati yake na Metacha aliyemaliza mechi za duru ya kwanza VPL akiwa na cleansheet 11

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’