Mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa amesema wanaendelea na jukumu la kuipeleka Yanga kwenye mfumo mpya wa uendeshaji
Bosi huyo wa zamani Simba amesema anatambua maadui wasiomtakia mema yeye pamoja na Yanga hawalali, lakini wamewabaini na muda si mrefu watawaumbua
"Bado tunaendelea na kazi ya kupanga na kuweka sawa mikakati. Maadui zetu hawalali pia, tumewabaini, tutawaumbua karibuni," aliandika Senzo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Kwa siku za karibuni kumevumishwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa Senzo ameondolewa Yanga

Makamu mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alikanusha tetesi hizo huku akimtaka Senzo aendelee kuchapa kazi
Mabosi wake wa zamani (Simba) wanaonekana kumuhofia sana Senzo wakifanya kila jitihada kuhakikisha anaondoka nchini
Walianza kwa kumfungulia mashitaka ya kuihujumu klabu hiyo, huku wakiwatimua baadhi ya watendaji wao waliokuwa karibu na Senzo
Inaelezwa hata taarifa feki kuhusu Senzo zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zinasimamiwa na watu hao
Β