Huu ni mwanzo tu, mazuri zaidi yanakuja - Saido

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jan 2021
Huu ni mwanzo tu, mazuri zaidi yanakuja - Saido

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza 'Antibiotic' amesema ni faraja kwake akiwa mchezaji wa Yanga kushinda taji lake la kwanza na kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria

Nyota huyo wa Kimataifa kutoka Burundi, amewaahidi mashabiki wa Yanga kuwa watarajie mambo mazuri zaidi kutoka kwake

Ntibazonkiza alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Simba mikwaju ya penati 4-3 baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Saido alicheza mchezo huo kwa dakika zote 90 na ndiye aliyefunga penati ya mwisho iliyoihakikishia Yanga ubingwa

Mwenyewe amesema alishiriki michuano hiyo akiwa hayuko fiti kwa asilimia 100 lakini kwa heshima ya wachezaji wenzake, viongozi na mashabiki aliamua kuwa sehemu ya kikosi kilichocheza fainali licha ya kuwa hakuwa amefanya mazoezi na timu kwa wiki tatu kutokana na majeraha

Tangu atue Yanga mwezi uliopita, Ntibazonkiza ameonyesha kiwango kikubwa. Nyota huyo aliibuka na tuzo ya mchezaji bora wa VPL mwezi Desemba, ameichezea Yanga michezo mitano na kuhusika kwenye mabao saba akifunga mabao manne na kuasisti mara tatu.

"Nafurahi kwa kufanikiwa kushinda taji langu la kwanza nikiwa na kikosi cha klabu ya Yanga, haya ni mafanikio makubwa kama mchezaji kwa kuwa kila mchezaji mkubwa anahitaji kuthibitisha uwezo wake kwa kupata mafanikio hususani kushinda mataji.

"Mimi siyo muongeaji sana, bali napenda kuonyesha uwezo wangu uwanjani na watu wanijaji kutokea huko, tumeanza na Mapinduzi na sasa mawazo yetu ni kuelekea kwenye mashindano mengine tutakayoshiriki," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’