Tanzania inakuwa timu ya kwanza kufungwa zaidi ya goli moja kwenye michuano ya CHAN 2020 inayoendelea nchini Cameroon baada kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Zambia
Stars ilikuwa na mchezo mzuri kwenye kipindi cha kwanza ikiwalazimisha Zambia suluhu hadi wakati wa mapumziko
Mambo yalibadilika kwenye kipindi cha pili Zambia wakifunga bao la kwanza kupitia mkwaju wa penati kwenye dakika ya 64 baada ya beki Shomari Kapombe kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari
Chabula akaongeza la pili kwenye dakika ya 81. Stars inahitaji kuchanga karata zake vyema katika michezo itakayofuata dhidi ya Namibia na Guinea ili kuweka hai matumaini ya kuvuka hatua ya makundi
ADVERTISE HERE