Jaji raia wa Uingereza ameteuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya shauri la rufaa ya Yanga dhidi ya mchezaji Benard Morrison
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wamepokea barua kutoka CAS kuwataarifa juu ya uteuzi wa Jaji huyo baada ya kuwa wamekamilisha malipo waliyopaswa kuyafanya kabla Januari 12 ili kesi hiyo iweze kusikilizwa
Jaji huyo anatoka jiji la Manchester huko Uingereza
"Tumepokea barua kutoka CAS ambayo imetutaarifu kuwa shauri letu dhidi ya mchezaji Bernard Morrison limepangiwa Jaji wa kulisikiliza. Jaji huyo anatoka Jiji la Manchester nchini Uingereza. Tunasubiri maelekezo zaidi kutoka CAS wakati shauri letu litakapoanza kusikilizwa," amesema
ADVERTISE HERE