Yanga Princess imemaliza duru ya kwanza ligi kuu ya Wanawake kibabe baada ya kuibamiza Alliance Girls mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza
Kama kawaida kinara wa mabao katika ligi hiyo Aisha Masaka ameweka kambani mabao mawili hivyo kufikisha mabao 15
Ushindi huo unaifanya Yanga Princess ifikishe alama 31 baada ya kumaliza mechi zote 11 za duru ya kwanza
Ushindi ni mechi 10, sare moja, wanakamilisha duru ya kwanza bila ya kupoteza mchezo kama ilivyo kwa kaka zao Yanga ambao nao wako kileleni mwa msimamo wa VPL wakiwa na alama 44
Tunasema hivi, huu mziki hauzimwi mpaka Mei...!
ADVERTISE HERE