Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi chake kimeanza mazoezi kujiandaa na ngwe ya lala salama ya ligi kuu ya Vodacom na michuano ya kombe la FA
Baada ya mapumziko ya siku 10, nyota wa Yanga walianza kujifua jana ambapo wachezaji wengine hasa wale waliosafiri nje ya nchi, wanatarajiwa kuwasili leo na kesho
Akizungumza baada ya siku ya kwanza ya mazoezi, Kaze amesema vijana wake wako vizuri akiwa na matumaini watarejea katika hali yao ya ushindani ndani ya muda mfupi
"Baada ya mapumziko ya siku 10, leo (jana) ilikuwa siku ya kuangalia hali za wachezaji walitumia vipi mapumziko. Tmeandaa mpango wa mazoezi ambao naamini utatusaidia kuwa tayari kuendelea na mazunguuko wa pili wa ligi pale mechi ya kwanza itakapofika," alisema Kaze
Aidha Kaze aliongeza kuwa nyota wawili Yacoub Songne na Sadio Ntibazonkiza waliokuwa majeruhi, wataungana na timu wiki hii wakati mshambuliaji mpya Fiston Abdul Razak naye ataungana na timu leo