Februari 13 ligi kuu ya Vodacom inarejea kukamilisha mzunguuko wa pili ambapo mabingwa wa kihistoria Yanga ambao wako kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, wataanzia kule mkoani Mbeya kuikabili Mbeya City
Kisha kufuatiwa na michezo miwili jijini Dar es salaam dhidi ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Vijana wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mechi hizo
Michezo yote iliyobaki haitakuwa rahisi lakini ni michezo ya hesabu kuhakikisha ubingwa unarejea Jangwani baada ya kupotea kwa misimu mitatu
Ni hitaji la Yanga kushinda ubingwa msimu huu ambapo tangu mwanzoni mwa msimu ni kipaumbele cha kwanza
GSM wamefanya uwekezaji mkubwa kwa kuboresha kikosi, benchi la ufundi pamoja na kambi nzuri ya maandalizi
Mwishoni mwa msimu uliopita, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alisema kuwa kama watakosa ubingwa msimu huu, basi watakaolumiwa ni wao GSM
Wametimiza wajibu wao kwani dalili zimeonekana mapema, Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu huku ikiwa imeweka kibindoni taji la michuano ya Mapinduzi iliyofanyika mwezi uliopita visiwani Zanzibar