Pichani washambuliaji Michael Sarpong na Fiston Abdul Razak wakiwa katika majukumu yao kwenye mazoezi ya kikosi cha Yanga yanayoendelea Kigamboni ndani ya Mji wa Kitalii, Avic Town
Hawa watu wamepania kwelikwali ligi itakaporejea Februari 13, kuna timu zijiandae 'kisaikolojia'
Akiwa na siku mbili tu tangu aanze kujifua na Yanga, Fiston tayari ameonyesha ni kiasi gani atawatesa makipa wa timu pinzani
Ni mchezaji anayefahamu wajibu wake ipasavyo linapokuja suala la kuzifumania nyavu
Ujio wake ni kama umemuongezea makali Sarpong ambaye anafahamu sasa analazimika kuipigania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza
Wananchi wajiandae kwa burudani ya aina yake ligi itakaporejea
ADVERTISE HERE