Senzo apongezwa kwa kuleta Wananchi Media Day

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2021
Senzo apongezwa kwa kuleta Wananchi Media Day

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said, amempongeza Mshauri wa Yanga Senzo Bartha kwa kubuni wazo na kuandaa Wananchi Medi Day tukio ambalo limefanyika leo katika viunga vya Avic Town, Kigamboni jijini Dar es salaam

Yanga imeandika historia nchini Tanzania leo kwa kuandaa tukio hilo ambalo limewakutanisha waandishi wa habari, wadhamini, viongozi na wachezaji wa klabu ya Yanga katika mji huo ambao Yanga imeweka kambi

Akizungumza kwa niaba ya GSM, Hersi amesema tukio hilo ni la kipekee na kwa hakika limewapa fursa wanahabari na wadau wa soka kuonana ana kwa ana na wanafamilia wa klabu ya Yanga na kupata nafasi ya kubadilishana mawazo

Aidha Hersi amesema GSM itaendelea kuisapoti na kuipambania klabu kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa

"Nampongeza Mr senzo Mbatha kwa kuanzisha tukio hili la Wananchi Media Day, pia tunafurahishwa na tunaridhishwa na namna timu inavyoendeshwa, namna uongozi wa klabu ya Yanga unavyofanya kazi"

"Tunawaomba mashabiki na wapenzi wa Klabu ya Yanga kuendelea kuisapoti klabu, sisi GSM tutaendelea kuisapoti na kuipambania klabu kwa asilimia Mia Moja, kama kushinda tutashinda pamoja na kama kupoteza tutapoteza pamoja," alisema

Nao wadhamini wakuu wa klabu ya Yanga, kampuni ya Sportpesa wameeleza kufurahishwa na tukio hilo wakieleza kuwa ni tukio la kihistoria kufanyika kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania

"Tumefurahishwa na klabu ya Yanga Sc kwa tukio waliloliandaa la Wananchi Media Day, ni tukio la Kihistoria katika soka la Tanzania na Yanga inakuwa muanzilishi wa tukio hili Zuri na la Kihistoria la kuwakutanisha Waandishi wa habari kuja kutembelea Training Camp ya Klabu," alisema Mwakilishi wa SportPesa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’