Baadae leo Wananchi wanakutana pale uwanja wa Azam Cpmplex, Chamazi kushuhudia mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya African Sports
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa moja kamili usiku
Huu ni mchezo wa kupasha misuli moto, yakiwa ni maandalizi kuelekea mikiki mikiki ya lala salama ligi kuu ya Vodacom
Vinara hao wa ligi watakuwa na nafasi ya kunoa silaha zao tayari kwa mapambano ya kuwania ubingwa
Hii ni mechi ambayo kocha Cedric Kaze anatarajiwa kuwatambulisha katika kikosi chake nyota wapya mshambuliaji Fiston Abdul Razak na mlinzi Dickson Job waliotua katika usajili wa dirisha dogo
Hawa African Sports sio wa kubeza, ni timu imara inayowania nafasi ya kupanda ligi kuu kutoka ligi daraja la kwanza
Mwishoni mwa mwaka jana walicheza na Simba na kuwalazimisha suluhu ya bila kufungana, mchezo ukipigwa hapo hapo Azam Complex
Hivyo ni kipimo kizuri kwa Yanga kabla ya safari ya mkoani Mbeya kuifuata Mbeya City