Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze ameeleza kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji wake mpya Fiston Abdul Razak katika mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, ulimalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0
Kaze alimuanzisha Fiston sambamba na Waziri Junior katika safu ya ushambuliaji
Kaze alisema Fiston alijitahidi kicha ya kuwa mgeni kikosini, lakini pia bado hayuko fiti kwa asilimia 100
"Huu ni mchezo wake wa kwanza kwenye timu, amejitahidi. Ni mchezaji mgeni, bado hajafanya mazoezi ya kutosha na hajafahamiana vyema na wenzake (uwanjani). Wachezaji wenzake nao wanahitaji kufahamu jinsi vile wanaweza kumchezesha"
"Sina wasiwasi nae, ni mchezaji mzuri ambaye naamini ataongeza kitu katika kikosi chetu," alisema Kaze
Akizungumzia mchezo wenyewe, Kaze amesema timu yake ilikosa bahati kwani walipoteza karibu nafasi saba za kufunga
Lakini amesisitiza kipaumbele chake hayakuwa matokeo, alihitaji kuona vile wachezaji wake watacheza baada ya kufanya mazoezi magumu kwa wiki mbili