Mabadiliko yataongeza uwajibikaji - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Feb 2021
Mabadiliko yataongeza uwajibikaji - Senzo

Mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa amesema changamoto zinazokabili vilabu vingi vya soka Barani Afrika zinatokana na kutokuwa na mifumo sahihi ya uendeshaji

Senzo anayesimamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji Yanga akiwa mshauri mkuu, amesema Mabadiliko yanayofanywa na Yanga yataongeza uwajibikaji wa viongozi katika masuala mbalimbali na yatakuwa mfano kwa wengine kujifunza

Wiki iliyopita FIFA iliiamuru Yanga kumlipa aliyekuwa mshambuliaji wake Amisi Tambwe malimbikizo ya madeni anayoidai klabu hiyo

Aidha FIFA ilitahadharisha kuwa Yanga itafungiwa kutosajili wachezaji kwa madirisha matatu kama hawatamlipa Tambwe katika kipindi cha siku 45

Jambo hili halikuwafurahisha mashabiki na wanachama wa Yanga kwani wanaamini upo uzembe uliofanyika hadi kupelekea Tambwe akalipeleka suala hilo FIFA

Senzo amesema kesi hii ni mfano wa umuhimu wa kuwa na mfumo bora wa uendeshaji ambao utaepusha changamoto za aina hii

"Utaona sababu kubwa ya klabu na GSM kusimamia mchakato huu wa Mabadiliko ni kutaka kuona klabu inaondoka katika eneo kama hili. Hili suala la Tambwe tunalishughulikia lakini hatutarajii kuona jambo kama hili linajitokeza tena," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
56m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’