Viwanja kwa ajli ya michezo ya nusu fainali na fainali ya mashindano ya kombe la shirikisho FA vimewekwa hadharani jana na kamati ya mashindano ya shirikisho la soka nchini TFF wakati wa uchezeshwaji wa droo ya kupanga michezo ya hatua ya 32 bora ya mashindano hayo
Tukio hilo la kuchezeshwa kwa droo ya kupanga michezo ya 32 bora lilifanyika mubashara kutoka studio za Azam TV jijini Dar es salaam ambao pia ni wadhamini wa mashindano hayo makubwa yanayotoa mwakilishi wa nchi kimataifa kwa upande wa kombe la shirikisho.
Katika michuano ya mwaka huu, mchezo wa fainali na michezo miwili ya nusu fainali itapigwa katika mikoa ambayo haina timu zinazoshiriki ligi kuu
Mchezo wa fainali utapigwa katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma wakati mechi mbili za nusu fainali zitapigwa mikoa ya Tabora na Ruvuma
Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora utatumika katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali na uwanja wa Majimaji Songea, utatumika katika mchezo wa pili a nusu fainali
Hata hivyo TFF wanapaswa kufanyia maboresho viwanja hivyo ili viweze kuwa na hadhi ya kutumika katika mechi hizo