Msafara wa kikosi cha Yanga utaondoka jijini Dar es salaam leo Alhamisi mchana kuelekea mkoani Mbeya tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa Jumamosi, Februari 13 uwanja wa Sokoine
Yanga itaondoka kwa usafiri wa Ndege ikiwa na msafara wa wachezaji 24 na viongozi 14, nane wakiwa wa benchi la ufundi
Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wa timu hiyo mkoani Mbeya wajitokeze kwa wingi uwanja wa Songwe kuipokea timu yao
"Kama kawaida yetu Wanachama, Wapenzi na Mashabiki tujitokeze kwa wingi kwenye uwanja wa ndege wa Songwe Kuwapokea na kuwalaki wachezaji wetu"
ADVERTISE HERE