Mastaa Yanga wazitaka pointi tatu za Mbeya City

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Feb 2021
Mastaa Yanga wazitaka pointi tatu za Mbeya City

Nyota wa Yanga wameapa kupambana kuhakikisha wanashinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City kuendelea kuweka hai malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu

Ni misimu mitatu sasa imepita tangu Wanayanga  washangilie ubingwa wa ligi kuu

Aidha kwa wachezaji ubingwa ndio kipaumbele cha kwanza. Ili kufanikisha hilo, Yanga inapaswa kushinda kila mchezo unaokuja mbele yake

Lengo ni kukusanya alama nyingi ambazo hesabu yake inaweza kutimia mwishoni mwa msimu na Wananchi kurejea katika utamaduni wao wa kubeba makombe

Kiungo fundi wa mabingwa hao wa kihistoria Feisal Salum 'Fei Toto' amesema wamesafiri mkoani Mbeya kuzipigania alama tatu, lengo lao ni kuhakikisha wanalifanikisha hilo

"Tunachofikiria sisi ni kupata matokeo mazuri dhidi ya Mbeya City. Kama timu tuna malengo na tutapambana ili tufanikiwe. Tunawaomba mashabiki wetu watuunge mkono na wasisahau kutuombea dua ili tufanikiwe," alisema

Naye mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari amesema wanafahamu mchezo dhidi ya Mbeya City hautakuwa mwepesi kama ilivyo mechi zote wanazocheza haziwi nyepesi lakini lengo lao ni kuondoka na ushindi

"Pamoja na ushindani uliopo, msimu huu malengo yetu ni ubingwa, hivyo ni lazima tuweze kukusanya pointi nyingi ikiwemo katika mchezo wetu unaofuata dhidi ya Mbeya City, tutapambana kufanikisha hilo"

Yanga wako mkoani Mbeya tangu jana, leo wakitarajiwa kukamilisha maandalizi ya mwisho katika uwanja wa Sokoine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’