Match Day : Mbeya City vs Yanga, uwanja wa Sokoine

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Feb 2021
Match Day : Mbeya City vs Yanga, uwanja wa Sokoine

Baada ya mapumziko ya michuano ya CHAN, vinara wa ligi kuu ya Vodacom Yanga leo wanarejea 'mzigoni' wakianzia kule mkoani Mbeya kwa mchezo dhidi ya Mbeya City

Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali. Mbeya City wamekuwa bora sana kila wanapocheza katika uwanja wa Sokoine

Hata hivyo, msimu huu Yanga tayari wamecheza katika uwanja huo dhidi ya Ihefu Fc na wakafanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-0

Timu hizi zilipokutana kule jijini Dar es salaam, Wananchi walilazimika kusubiri mpaka dakika ya 87 kushangilia bao la Lamine Moro ambalo liliwahakikishia alama tatu muhimu

Kila kona ya mji wa Mbeya utashuhudia shamrashamra za mashabiki wa Yanga ambao wanaamini timu yao leo itaendeleza wimbi la ushindi lengo likiwa kufanikisha kutwaa ubingwa msimu huu

Katika mchezo huo Yanga itamkosa nyota wake muhimu Saido Ntibazonkiza ambaye amebaki jijini Dar es salaam akisumbuliwa na matatizo ya misuli

Aidha kocha Cedric Kaze pia amethibitisha kuwa mshambuliaji Yacouba Songne na beki Dickson Job watakosekana kwa kuwa hawako fiti

Hata hivyo fundi raia wa Angola Carlinhos yeye anarejea baada ya kukosekana kwa muda mrefu

Ni mchezo ambao hesabu za Wananchi wamezielekeza katika kukusanya alama zote tatu

Lakini wanatarajiwa kukumbana na upinzani mkali kutoka kwa Mbeya City ambao wanapokuwa hapo Sokoine mara nyingi wanakuwa wagumu sana kufungwa na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’