Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amewashushia lawama waamuzi wa mchezo dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1
Tatizo sio Yanga kutoa sare, ipo changamoto kubwa kwa waamuzi wanaochezesha mechi za ligi kuu hasa Yanga inapocheza na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine
Imekuwa kawaida kwa Yanga kukutana na maamuzi ya ajabu katika mechi zao wanazocheza na Mbeya City hapo Sokoine
Achana na mkwaju wa penati ambao Mbeya City walipewa dakika za majeruhi, Yanga ilinyimwa penati dhahiri kwa madhambi aliyofanyiwa Kaseke mapema
Angalia baadhi ya matukio kama mpira wa kurushwa watu wanapiga na mguu na mwamuzi hana alilofanya
Feisal alifanyiwa madhambi ya hatari sana lakini ajabu hakuna hata kadi iliyotolewa
Kaze ameeleza kuchukizwa na kile alichokiona leo akihisi kuwepo hujumu ya waziwazi ili timu yake isiweze kushinda
Amesema matokeo ya mchezo huo hayawezi kuwakatisha tamaa, watapambana katika michezo ijayo ili wahakikishe wanatimiza malengo waliyojiwekea